Job 2:8-13

8 aNdipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu.

9 bMke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”

10 cAkamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavu
Mpumbavu hapa ina maana ya kupungukiwa maadili.
yeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.

Marafiki Watatu Wa Ayubu

11 eBasi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji. 12 fWalipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua. Wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao. 13 gKisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba usiku na mchana. Hakuna yeyote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.
Copyright information for SwhKC